Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombajikazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 04-05-2024 na tarehe 11-02-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenyekanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada yanafasi kupatikana.
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katikaOfisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu chaDodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya sikusaba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa nawahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwaMwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwana vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ilivihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapokatika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisitekuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
MUHIMU:
Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulishokwa ajili ya utambuzi;
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya Udereva.